Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MAKOSA MAKUBWA WANAYOYAFANYA WANAWAKE LINAPOKUJA SUALA LA KUPENDA

Je wewe ni mtu wa kupenda ghafla, yaani
mwanaume anapokutamkia kwamba
anakupenda huwa unamuamini kwa kiasi
gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini
na kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na
kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya
kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla
ya kuamua, jipe muda kwani hakuna jambo
lililo jema kama subira linapokuja swala la
kupenda. Subira itakuepusha kupoteza
muda wako katika mahusiano ambayo
hayana mashiko wakati dhamira yako
ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa
muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo
sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano
huo kuna gharama kubwa na kunaweza
kukusababishia matatizo mengi yakiwemo
ya kiafya.
Hapa chini nitajaribu kueleza makosa
kadhaa ambayo wanayafanya wanawake
linapokuja swal la kupenda:
1.Kumbadili mtu awe vile utakavyo:
Usije ukajidanganya kwamba unaweza
kumbadilisha mtu mzima na akili zake.
Kama umepata mwanaume ambaye kwa
mtazamo wako unamuona ana sifa
muafaka lakini anatabia ambazo huzipendi
kwa mfano ulevi au kuvuta sigara vitu
ambavyo vinakukera sana, usije
ukajidanganya kwamba unaweza
kumbadilisha na akaacha tabia hizo,
anaweza kuacha kwa muda tu ili kukuvuta
ukiingia kingi imekula kwako, tabia hiyo
inaweza kujirudia. Ni vyema kama kuna
tabia ambazo umezipenda lakini zipo
ambazo huzipendi kutoka kwa mwenzi
wako, basi weka uzingativu kwenye zile
tabia unazozipendfa na zile usizozipenda
achana nazo, kama ataamua mwenyewe
kuziacha sawa lakini kama akiamua
kuendelea nazo, basi zisikuumize kwani
unaweza kujikuta ndoa yako inakuwa na
migogoro isiyokwisha kwa sababu ya
kuonekana una ghubu kwa kujaribu
kumbadilisha mwenzi wako na mwisho
wake upendo unakuwa haupo na kisirani
katika ndoa kinaongezeka. Kitendo cha
kuonekana kuwa na ghubu kinaweza
kumuingiza mwanaume katika tabia
nyingine mbaya ya kutotumia muda mwingi
kukaa nyumbani kwake na kutafuta
kampani nyingine, kama akipata kampani
ambayo siyo nzuri anaweza kuangikia
katika nyumba ndogo ambayo itamkubali
bila masharti.
2.Njoo tuishi:
Unaweza kukutana na mwanaume ambaye
ana nyumba nzuri au amepanga nyumba
nzuri na ana kila kitu ndani pamoja na
usafiri, anakuwa mwepesi kukupa funguo
za nyumba yake ili uhamie muishi pamoja,
lakini haweki msimamo wake wazi
kwamba ana matarajio gani na wewe.
Kabla ya kukubali kupokea funguo na
kuhamia kwake jiulize kama unampenda
kwa dhati au umekubali kwa sababu ya
nyumba yake nzuri. Kumbuka nyumba na
vitu vingine vinavyotizamika kwa macho
(material things) havina mashiko linapokuja
swala la kupenda. Kupenda kunahusisha
vitu vya ndani kama vile kupenda kwa dhati
bila masharti wala kuangalia sifa za nje,
kuwa na amani moyoni kila umwonapo
mpenzi wako, kuwa na furaha wakati wote
mnapokuwa pamoja, kupatwa na msisimko
wa mapenzi kila umwonapo au usikiapo
sauti yake nk. Lakini kama utamkubali
mwanaume kirahisi kwa sababu tu
kakukabidhi funguo za nyumba yake
wakati huna mapenzi ya dhati ni janga
kubwa kwa sababu hivi vitu vya nje
vinaweza kutoweka kirahisi, sasa je
ikitokea si mapenzi nayo yatakuwa
yamekwisha? Kumbuka kwamba kile
kilichokupeleka kwake hakipo.
3.Amekuwa ni liwazo kwako
Liwazo linaweza kuwa sehemu ya mapenzi
lakini hivi vitu haviendi pamoja. Unaweza
kuwa na mwanaume ambaye mnapendana
na mnakamilishana hii ni tofauti na
mwanaume unayempenda na ukamgeuza
kuwa liwazo pale unapohisi upweke. Jiulize,
je ni kwamba mnapendana na mnafurahi
kuwa pamoja au unampenda kiasi kwamba
huwezi kuishi bila uwepo wake. Hapa
nazungumzia utegemezi wa kihisia, yaani
unakuwa king'ang'anizi mpaka mwanaume
anakuona kero, badala ya kufurahia
mahusiano yenu mwanaume anakuona
kuwa ni kero kutokana na kuwa tegemezi
wa kihisia. Hakuna mwanaume anayependa
mahusiano ya aina hii anachoka haraka
kihisia na atajitahidi kwa kila namna
kukukwepa na ikiwezekana kukutosa na
kutafuta ustaarabu mwingine jambo
ambalo litakuumiza sana.
4.Mwanaume king'ang'anizi:
Mwanaume kutongoza na kukataliwa siyo
jambo linalowashughulisha sana kwao
kujaribu na kukosa ni sehemu ya maisha,
lakini lipo suala la kung'ang'ania, yaani
mwanaume kumfuatilia mwanamke kwa
hali na mali na kujitoa ili kuhakikisha
anampata mwanamke anayemtaka. Huu ni
mtego wa mapenzi, kwani kwa mwanaume
kung'ang'ania na kufuatilia mwanamke
kwa muda mrefu bila kuchoka hata
asumbuliwe kiasi gani haimaanishi
kwamba mwanaume huyo amempenda
mwanamke huyo. Wakati mwingine ni
matamanio tu ndiyo yamemsukuma
kutokana na sifa za nje alizo nazo
mwanamke huyo. Kupenda kwa
mwanaume kunahusisha zaidi sifa za nje
kuliko za ndani na ndiyo maana mapenzi ya
aina hiyo hayadumu yanaanza kama kichaa
na kuyeyuka ghafla kama kipande cha
barafu juani. Pale mwanamke anapokutana
na mwanaume king'ang'anizi na asiyekubali
jibu la hapana, kabla ya kukubali ajiulize
kama anakubali kuwa na mahusiano na
mwanaume huyo kwa sababu amempenda
kwa dhati au kwa sababu ya
uking'anga'nizi wake? Kumbuka kwamba
wapo baadhi ya wanawake wanaweza
kumkubali mwanaume tu kwa sababu
amemfuatilia sana, anajiwa na huruma
anakubali kuwa na mausiano naye siyo kwa
sababu amempenda bali kwa sababu ya
huruma. Ni vyema ukajiuliza kama na yeye
atathamini huruma yako au akishapata
alichokitaka atakugeuka na kuwa mwiba
mchungu kwako? Tafakari na chukua
hatua.
5.Baada ya kupanda mbegu mmea
ukachipua
Umekuwa na uhusiano na mwanaume
huyu kwa muda mrefu, lakini hakuwahi
kukutamkia kwamba ana matarajio gani na
wewe kuhusiana na swala la ndao, ghafla
unakoma kuziona siku zako… Mimba hiyo!
Je unafanyaje?
Kwanza naomba ufahamu kwamba, kupata
mimba haimaanishi ndiyo kuolewa. Hili ni
kosa ambalo wanalifanya wanawake wengi
tena wa kiwango cha kutosha, wanaamini
kwamba kubeba mimba kutawahakikishia
kuolewa na mwanaume aliyempa ujauzito.
Kwa huku kwetu sheria haziwabani sana
wanaume linapokuja swal la kulea mimba
na matunzo ya mtoto kwa hiyo mwanaume
kumtosa mwanamke aliyebeba ujauzito
siyo jambo la kushangaza. Wanawake
ambao ni single mother wanajua kuhusu
jambo hilo. Kwa hiyo kama unabeba mimba
fanya hivyo ukiwa umejiandaa kujitwika
changamoto zitakazojitokeza na usije
ukajifariji ukidhani kutakuwa na masaada
kutoka kwa mwenzi wako, utakuwa
unajidanganya. Kama akikubali mfunge
ndoa sawa, kama akikubali kulea mimba na
mtoto atakeyezaliwa pia ni sawa, akikataa
wala usivunjike moyo, simama imara na
songa mbele na maisha kwani kuzaa kabla
ya ndao siyo mwisho wa maisha, yapo
maisha tena mazuri sana ukiwa na
mwanao. Kwanza unaye mtu wa
kukuliwaza, na pili utakuwa umajihakikishia
kwamba wewe si mgumba, na tatu leo na
kesho umekuwa mtu mzima unaye wa
kukushika bega kuliko kutegemea ndugu
zako.
6.Pesa inapokuwa sehemu katika kupenda.
Wapo baadhi ya wanawake kabla ya
kumkubalia mwanaume wanaangalia
anamiliki kitu gani, amesoma kwa kiwango
gani, ana kazi ya aina gani, anafanya
shughuli gani, anazo fedha za kutosha au
yuko katika mazingira ya utafutaji
yanayoashiria neema huko mbeleni. Sikatai
kwamba wanawake kabla ya kumkubali
mwanaume wanataka kujihakikishia
usalama, na kama nilivyowahi kusema hapa
mara nyingi kwamba usalama kwa
mwanamke maana yake ni mtu kuwa na
fedha, tofauti na zama za kale za mawe
ambapo uwindaji na kilimo kilimuweka
mwanaume shupavu katika nyanja hizo
kukimbiliwa na wanawake. Siku hizi hayo
hayapo, fedha imekuwa ni njia ya mkato
katika kupata kila kitu. Kwa mwanamke
fedha ni mtego umnasao kama panya na
kipande cha nguru mtegoni. Siku hizi ukiwa
na fedha una uwezo wa kumpata
mwanamke umtakaye, fedha imekuwa
kama tufani, inabeba waliomo na
wasiokuwemo, hata wale watakaotokwa
na povu kupinga hoja hii, nadhani
hawajapata bahati ya kukutana na
wanaume wenye fedha, laiti wangepata
wasingeweza kusimama hapa na kupinga
hoja hii. Kwa ushauri tu, si vibaya kuangalia
mwanaume mwenye muelekeo wa kutafuta
lakini hicho kisiwe ni kigezo namba moja,
kwani kama akikuonyesha sifa hizo kabla
ya kuingia kwenye uhusiano kisha ukaingia
na baadaye ukagundua mwanaume huyo si
mali kitu wenyewe mnaita mwanaume
suruale, utaumia sana.
7. Uzuri wa kitandani
Ninaposema uzuri wa kitandani
namaanisha kuridhishana katika tendo la
kujamiiana, kwa kawaida wanawake ndiyo
wahanga wakubwa linapokuja swala la
njaa chumbani, wao ndiyo kwa asilimia
kubwa hawaridhishwi na wenzi wao katika
tendo. Siyo kwamba waume zao wana
udhaifu, la hasha, inawezekana wanazo
nguvu kama za simba, lakini kwa kawaida
tendo la kujamiiana haliwi zuri eti kwa
sababu tu mwanaume anazo nguvu kama
za simba, bali inahitaji usanii na utundu
ukiwemo werevu wa kihisia kuweza
kumfikisha mwanamke kileleni. Wanaume
wengi kwa sababu ya mazoea wanadhani
swala la kumfikisha mwanamke kileleni ni
kutwanga kwa kutumia msuli. Si kweli hata
kidogo, ni kumuandaa mwanamke kwa
maneno matamu kabla hata ya kuelekea
kitandani. Kwa hiyo wapo wanaume wenye
ufundi huo linapokuja swala la kujamiiana,
nia mafundi hodari wenye uwezo wa
kuwafikisha wenzi wao peponi, lakini
inawezekana katika maeneo mengine ya
kimaisha wakawa watupu kabisa. Siyo
wawajibikaji, wanyanyasaji wakubwa,
hawana staha, hawawaheshimu wenzi wao
na ni wenye vurugu kichwani. Wakati
mwingine mwanamke anaweza kunasa
kwa sababu hiyo tu, ya ufundi wa
kitandani, lakini akajikuta anaishi katika
machungu kutokana na kutothaminiwa na
kunyanyaswa kupita kiasi. Kinachomuweka
si kingine ni ile starehe ya muda mfupi
wawapo kitandani tu basi. Kuna haja ya
kujiuliza, Je ni kitu gani hasa
kinachokufanya umpende mwenzi wako?
Kama utamkubali na udhaifu wake na una
uwezo wa kuhimili hizo tabia zisizofaa kwa
maana kwamba hazikuumizi kihisia (kitu
ambacho si rahisi sana kwa wanawake) ni
sawa, lakini kama huwezi, sikushauri
kuingia katika uhusiano wa aina hiyo,
kwani ni kujitafutia kaburi la mapema.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top