Rio de Janeiro, Brazil WENYEJI
Brazil leo Alhamisi watakuwa na kibarua pevu cha kuhakikisha wanaanza
vyema michuano ya Kombe la Dunia ambapo wanatarajiwa kufungua pazia kwa
kumenyana na timu ya taifa ya Croatia kwenye Uwanja wa Rio de Janeiro
mjini hapa.
Ikumbukwe
kuwa Croatia inayonolewa na Niko Kovač, haijawahi kuifunga Brazil zaidi
ya kuambulia sare na vipigo hivyo leo inatarajiwa kuwa mechi ya kukata
na shoka inayotarajiwa kuanza mishale ya saa 5 usiku.
Mara
ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye michuano ya Kombe la Dunia
mwaka 2006 iliyofanyika nchini Ujerumani, Brazil iliichapa Croatia bao
1-0 lililotupiwa kimiani na kiungo Ricardo Kaka ambaye mwaka huu
hajaitwa katika timu hiyo.
Tayari mshambuliaji tegemeo wa Brazil, Neymar dos Santos, amesharejea uwanjani na ameahidi kufanya makubwa kwenye mechi ya leo.
Kwa upande wa Croatia kupitia kwa kocha wao Niko amesema kikosi chake
hakitapaki basi kwenye mchezo wa leo ambao wenyeji wanapewa nafasi
kubwa ya kushinda.
Wachezaji tegemeo Brazil: Neymar, David Luiz, Dani Alves, Fred, Ramires, Paulinho, Marcelo, Willian, Hulk, Dante, Thiago Silva na kipa Julio Cesar.
Wachezaji tegemeo Croatia: Darijo Srna, Dejan Lovren, Vedran Corluka, Danijel Pranjic, Luka Modric, Mario Mandzukic, Ivica Olic, Eduardo.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment