Waweza kuona nacheka ukadhani labda nimejawa na furaha, kumbe nafsi yangu imejaa karaha, imekereheka kama siyo kukereheshwa.
Kuna watu wengine kwa kweli kila kitu watende wao wakitenda wenzao huwa mwao, hutaka kuicheza ngoma hata kama siyo ya kwao, upo?
Hivi inaingia akilini mama mtu mzima kutaka kuingilia ndoa ya mwanaye? Tuchukulie mfano ni wewe mama ungekuwa na mtoto wa kike, ndoa yake ikawa inaingiliwa na mzazi mwenzako ungefurahi?
Nalisema hili kwenu nyie wenye tabia hii kwa kuwa huu ndiyo mwarobaini wenye ladha chungu, lakini ndani yake unapata dawa ya kutibu maradhi yako ya nyongo.Kwa nini leo nimeamua kuyasema haya? Jamani kuna shoga yangu mmoja kanijia mikono kichwani machozi churuchuru nikadhani labda amefiwa, alichonieleza nilibaki mdomo wazi kama siyo kupigwa na bumbuwazi.
Eti, mwanaye amekuwa akiendeshwa na mkewe kama gari bovu. Yaani mkwewe amekuwa ndiye kinara wa nyumba na mtoto wake hafurukuti wala hatikisiki.
Kila siku mama anamwambia mwanaye ubaya wa mkewe lakini mtoto wala hajali, maneno yanaingia sikio hili yanatokea lile, hasikii kitu juu ya mkewe.
Siku moja, shoga yangu akapewa na mwanaye maneno makavu, kuwa hawezi kuachana na mkewe kama anavyotaka yeye, hilo likamuuma mpaka akaamua kuja kuniangushia kilio.
Mmh, makubwa limao alambe mwingine wewe ukunje uso kama ngozi ya goti, leo nataka niwaeleze nyie kina mama mnaokosa kazi na kufuatilia ndoa za watoto wenu, jamani acheniii.
Hamuoni aibu, mama mkwe kuacha kazi na kuwa kiguu na njia kufuatilia ndoa za watoto wenu kama mkia wa ng’ombe. Kwanza kwa mila na desturi za Kitanzania ni matusi kufanya hivyo.
Mama mtu mzima huna kazi, unafuatilia nyendo za mkweo, jioni mwanao akirudi unampa ‘full data’, cha ajabu mwanao haoneshi chochote kutokana na madai yako, unakasirika.
Mwanao wa kumzaa mwenyewe akikupuuza unamuona hafai na hana maana, unaanza kuzunguka mitaani na kusema kuwa, mwanao hajaoa bali kaolewa.
Ni jambo la kushangaza kwa mtu mwenye akili zake na aliyedumu katika ndoa kufanya ujinga huo.
Tunajua kwamba kuna wazazi walioshindwa kuziongoza ndoa zao kwa kukosa uaminifu, lakini leo ndiyo hao hao wanaokosa uso wa haya na kuanza kufuatilia maisha ya wakwe zao kisha kupeleka umbeya kwa watoto wao.Eti, watoto wao wakikataa ushauri wao wanataka kuwatolea radhi, mmh! Jamani nyie nani aliwatolea radhi? Mbona yenu mengi tunayajua lakini hatusemi?

Siye
tumenyamaza kwa kuelewa kwamba ndoa ni siri ya watu wawili, tunafahamu
pia kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho wake, kwa nini tutake kuitwa
wachawi kwa jambo ambalo ukweli unaweza kubainishwa na mhusika
mwenyewe?
Heee! Kama mke na mume kuna anayefanya uchafu ni mmoja kati yao ndiye anayeweza kuubainisha kwa kuwa wote wana macho watayaona na kutoa hukumu bila kumlaumu mtu yeyote ya nini siye tuyaingilie?
Tafadhali, shoga usiwe kimbelembele kama mfuko wa shati kutaka kuvunja ndoa ya mwanao, unajua mwanao anafanyiwa nini na mkweo? Unajua analishwa nini? unajua anapumbazwa kwa pumbazo gani? Alaaaa! Acha ushakunaku.Wewe kama ungefuatiliwa hivyo ndoa yako ingedumu? Yako ni yako na ya wenzako pia yako.Napenda kukwambia wewe unayebinua midomo kama samaki chuchunge na wenzako kuwa msipende kuingilia mambo ya watu wanaojifunika shuka moja, mtakuja kupatwa na aibu!
Yangu kwa leo ni hayo, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.

Post a Comment