Baadhi ya viongozi wanaowania urais nchini Malawi
Rais Joyce Banda wa Malawi 
ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza
 matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi 
uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na 
kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba 
yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.
chanzo; BBC. 
Post a Comment