Arsene Wenger ameongeza miaka mitatu Arsenal.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameongeza mkataba wa miaka mitatu
kubaki klabuni hapo. Atakuwa Arsenal mpaka mwaka 2017 kwa mkataba wa
pauni milioni 24 sawa na bilioni 66.9 za Tanzania.
Wenger baada ya kutwaa Kombe la FA.
Kocha huyo aliyetwaa Kombe la FA baada ya ukame wa makombe kwa miaka tisa, amepatiwa pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili.Wenger mwenye miaka 64, alidaiwa kuwa angeondoka klabuni hapo kama angeshindwa kutwaa kombe lolote msimu huu, jambo aliloliepuka kwa kutwaa Kombe la FA kwa kuwafunga Hull City katika fainali iliyopigwa Wembley.
Straika wa timu hiyo, Theo Walcott alitweet katika akaunti yake yaTwitter kuwa ni habari njema, baada ya bosi huyo kusaini.
Post a Comment