NI laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo
vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
Tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria, Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
Likishuhudia tukio hilo, Ijumaa Wikienda ambalo lilijipenyeza ndani ya nyumba, lilifuatilia kila aina ya tukio huku likifikisha ripoti kwa mkuu wake ambaye alikuwa ofisini akipokea matukio ya Live Dijitali.
Ndani ya ukumbi huo lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
Kingine kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka mipaka.
Tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria, Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
Likishuhudia tukio hilo, Ijumaa Wikienda ambalo lilijipenyeza ndani ya nyumba, lilifuatilia kila aina ya tukio huku likifikisha ripoti kwa mkuu wake ambaye alikuwa ofisini akipokea matukio ya Live Dijitali.
Ndani ya ukumbi huo lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
“Duh! Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii
ni Kwaresma, ni full laana hebu angalia Husna Maulid, Sajent (Husna
Idd) na Davina (Halima Yahya) wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi
‘makufuli’ yanaonekana,” alisema mwanadada mmoja.
Katika hatua nyingine, mwanaume tata
anayejulikana kwa jina la Agrey alivua nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha
alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha staili mbalimbali za ukataji wa
mauno.
“Tobaa… jamani mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii mmoja wa Kundi la Vituko Show.Kingine kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka mipaka.
Post a Comment