Mrembo huyo alitanabahisha kuwa, katika sherehe hiyo iliyowakusanya warembo mbalimbali, walialikwa wanawake maalum kwa kazi ya kumfunda Bi. harusi ambao walitakiwa kumfundisha mwanandoa huyo mtarajiwa (kwa wakati huo) namna alivyotakiwa kuishi na mume wake.
“Ile pati ilikuwa Bride Shower ya rafiki yangu (anamtaja jina) na wale wanawake waliokuwa wakicheza uchi walialikwa kwa lengo la kumfunda Bi. Harusi tu na si kucheza wakiwa uchi, kucheza kwao uchi waliamua wenyewe baada ya kupandisha midadi na sisi tulishindwa kuwazuia,” alisema Jacqueline.
Aliongeza kuwa, msichana aliyeandaa sherehe hiyo ni mtu mwenye maisha yake mazuri na anayejiheshimu kiasi kwamba asingeweza kuandaa shughuli hiyo haramu kisha kuwaalika marafiki zake anaowaheshimu.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta msichana aliyeandaa sherehe hiyo ya kifuska ili kuizungumzia lakini, simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Hata hivyo, baadhi ya watu walioshuhudia picha hizo kupitia gazeti dada la hili (Ijumaa Wikienda) walielezea kukerwa kwao na vitendo hivyo huku wakisema kuwa, ndivyo vimekuwa vikichochea kwa kiasi kikubwa kuenea kwa kasi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini.
“Jamani hata kama ni kicheni pati ya kumfunda mwali ndio wanawake wavue nguo na kucheza uchi huku wenzao wakichekelea na kuwapiga picha? Hivi jamii inaelekea wapi?” Alihoji Mama Zuhura mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam na kuongeza:
“Huku ni kudhalilishana na kama tutashindwa kuvivalia njuga vitendo hivi tujue tu kwamba hatutaweza kutimiza ule msemo wa Rais Kikwete wa ‘Tanzania bila Ukimwi inawezeka”.
Naye Shaban Kisuda wa Kiwalani jijini Dar es Salaam ameitaka serikali kuhakikisha wote wanaoshiriki katika kupiga ama kupigwa picha chafu wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
“Imefika wakati serikali iamke na iwashughulikie ipasavyo wote watakaobainika kushiriki katika vitendo hivyo vya kifisadi ili kuweza kuinusuru nchi yetu,” alisema Shabani.
Siku chache zilizopita Gazeti la Ijumaa Wikienda lilinasa na kuandika habari kuhusu mkanda wa video uliokuwa ukiwaonesha wanawake wa kitanzania wakicheza uchi huku wenzao na mwanaume mmoja wakipiga picha tukio zima.
Aidha, baada ya habari hiyo kuandikwa wahusika akiwemo Jacqueline waliibuka na kutoa ufafanuzi.
Hata hivyo, gazeti hili katika uchunguzi wake limebaini kuwepo kwa kasoro za wazi za sherehe hiyo ikiwemo wahudumu wa kiume kuruhusiwa kujumuika nao kinyume na taratibu za kicheni pati zilizozoeleka za kutoa mafunzo sahihi ya kuishi na mume.
Gazeti hili linalaani vikali vitendo hivyo na kuiomba serikali pamoja na taasisi husika kuhakikisha vitendo vinavyoathiri utamaduni wa kitanzania vinakomeshwa
Post a Comment