WAKATI
fulani unatakiwa kujihakikishia kuwa, mke au mume uliyenaye anakuwa
wako wa maisha yako yote. Kuapa tu mbele ya viongozi wa dini, kuwa
atakuwa wako, haitoshi! Kuna mengi zaidi ya kufanya.
Kazi
ya viongozi wa dini, mila au serikali ni kuwaunganisha tu. Kazi yao
humalizikia hapo, sasa suala la furaha ya ndoa ni kazi yenu wenyewe kama
wanandoa mkiwa ndani.
Ndugu
zangu, hivi umeshawahi kujiuliza; kwa nini mwanandoa anatoka nje?
Anafuata nini? Unajua unaweza kushangaa, ukiambiwa fulani anatoka na
mwanamke mwingine nje, wakati mke wake ni mzuri wa umbo, sura na tabia.
Watu
wakimwangalia wanamsumbua kila kukicha, wanaota ni lini watampata japo
kwa muda mfupi tu! Lazima ujiulize swali hili. Lakini hata wewe ambaye
labda umeshatoka nje au upo katika fikra hizo, lazima ujiulize,
unatafuta nini nje?
Mume/mkeo
ana kasoro gani? Nini tatizo? Nawe ambaye mwenzi wako ametoka nje na
una hakika na jambo hilo, inakupasa pia ujiulize na upate majibu ya
swali hilo. Kwa nini ametoka nje? Kuna nini huko nje ambacho wewe humpi?
Rafiki
zangu, asikudanganye mtu, tatizo kubwa kabisa huanzia katika kupoteza
hisia. Ukiwa na mwenzi wako, yakafanyika makosa na likatokea tatizo la
kupotea kwa hisia za mapenzi, ndiyo chanzo cha yote hayo.
Hakuna
kanuni za moja kwa moja za mapenzi ndugu zangu lakini yapo mambo ambayo
kiukweli kama yakizingatiwa vizuri, msisimko wa mapenzi huongezeka na
kujikuta ukizidi kumuona mwenzi wako mpya kila siku.
TATIZO HUANZIA HAPA
Wengi
huwa hawapati muda wa kufikiri na kutafakari juu ya jambo hili, lakini
furaha ya mtoto wa kwanza, wakati mwingine hugeuka kero na msumari
katika ndoa.
Wote
hufurahia mtoto wao mpya lakini mama asipokuwa makini ndiyo kipindi
ambacho anaweza kujikuta akipoteza msisimko wa tendo kwa mumewe. Kwa
kawaida, mwanamke akishajifungua na muda wa kukutana na mumewe ukifika,
mshawasha wake huwa wa juu zaidi.
Ni
kipindi ambacho mwanamke humhitaji mumewe kwa muda mrefu zaidi.
Atapenda awahi kurudi nyumbani, wale pamoja na kulala mapema ili aweze
kufurahi naye.
Tatizo
linakuja katika utaratibu mpya wa maisha baada ya kujifungua. Baadhi ya
wanawake hujisahau na kuanza kufanya mambo yanayopunguza msisimko bila
kujua.
Bahati nzuri ni kwamba, wakielezwa huelewa haraka sana. Hebu twende tukaone zaidi...
MAPENZI KUHAMIA KWA MTOTO
Kwanza
kabisa mwanamke akipata mtoto hujikuta akimpenda zaidi mwanaye kuliko
mumewe. Si kwamba hampendi mume wake tena lakini mapenzi kwa asilimia
kubwa kipindi hiki huhamia kwa mwanaye.
Mwanamke
anaweza kukesha usiku mzima, mwanaye akiwa pembeni yake na kumwacha
mumewe peke yake. Hili ni tatizo na husababisha kupunguza msisimko wa
mapenzi. Ni jambo hatari ambalo linaweza kusababisha mume kufikiria kuwa
na mwanamke mwingine wa nje.
Si
ajabu kichwani anaamini hafanyi makosa bali anakuwa na mwanamke wa muda
kwa ajili ya kumpisha mkewe amlee kwanza mtoto wao. Acha kujidanganya
rafiki, hilo ni kosa kubwa sana. Kwenye ndoa, usaliti ni sumu!
Wiki ijayo tutamalizia mada yetu.
Post a Comment