Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ISABELA AWAANGUKIA WATANZANIA

MSAMAHA!  Baada ya hivi karibuni kuvua nguo na kuonesha sehemu nyeti hadharani, msanii wa muziki na filamu Bongo, Isabela Mpanda ameibuka na kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo hicho kichafu alichokifanya.

 
Msanii wa muziki na filamu Bongo, Isabela Mpanda.
Akichonga na gazeti hili, Isabela alisema ameumia sana baada ya kuona picha akiwa ameacha sehemu zake nyeti nje hivyo anawaomba Watanzania wamsamehe kwani hakuwa akijua alichokuwa anakifanya kwa sababu ya ulevi.
“Naomba Watanzania waliokerwa na kitendo cha kuvua nguo hadharani wanisamehe kwani haikuwa akili zangu wala sikufanya kwa makusudi ila pombe ndizo zilizoniponza,” alisema Isabela.
Isabela aliacha nje sehemu nyeti katika kitchen party ya Vanitha Omary iliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Mawela, Dar.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top