Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HATIMAYE BATULI, STEVE NYERERE WAPATANA

IMEKAA poa sana! Lile bifu lililotia fora kwa wasanii wa filamu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ huku kila mmoja akiapa kutopatana na mwenzake, hatimaye limekwisha siku chache baada ya kifo cha msanii mwenzao, Adam Philip Kuambiana.

 
Wasanii wa filamu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ wakiwa katika picha ya pamoja.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walimaliza tofauti zao kutokana na kifo cha ghafla cha Kuambiana hivyo wakaamua wenyewe kuyamaliza kwani wameona maisha ni mafupi.
“Steve na Batuli kwa sasa wameshamaliza tofauti zao, wamepatana, wanaelewana vizuri sana na ni baada ya kifo cha Kuambiana ndipo walikaa wakaamua kuzungumza na kumaliza tofauti zao,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika ambapo Batuli alithibitisha kwamba ni kweli amemaliza tofauti zake na Steve na sasa wameanza maisha mapya kwani amegundua maisha ni mafupi na kifo kinakuja muda wowote.
Kwa upande wa Steve Nyerere alikuwa na haya ya kusema: “Mimi ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity na nilishasema nitamaliza tofauti zote yaani mabifu yote yataisha kwa sababu mimi ni kiongozi na mfano wa kuigwa nimemaliza bifu na Batuli naamini na hayo mengine yataisha, huu ni mwanzo tu.”

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top