Sisi maaskofu na wachungaji kutoka
makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa
wa Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015
alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka
kwenda kujibu shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.
Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?
Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya
kupata taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na
walinzi wake waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia
wamekamatwa kwa tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.
Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale
waliokuwa naye akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale
wale wanatuhumiwa kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni jambo la kushangaza na lisiloingia
akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima
kama angekua na nia hiyo angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo
wa kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa
ya Kipentekoste ambao alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.
Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna
polisi anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi
kutoroshwa leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi?
Mbona hii inastaajabisha?
Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa
kesi hii inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu
Gwajima kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo
ila mtu mmoja aitwaye Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa
Aboubakar sio MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha
ameumizwa kiasi gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada
yake ya Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi
tena mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Na mwandishi
F.A.K
30/03/2015
F.A.K
30/03/2015
Post a Comment