MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa inaendelea na vikao vyake huku leo kesi ya ya mauwaji ya mwanahabari mkoani Iringa Daud Mwangosi inayomkabilia mtuhumiwa wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Iringa (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573 inataraji kuanza kusikilizwa kwa upande wa mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao.
Kesi
hiyo inayoanza leo inaanza kusikilizwa leo Feb 12 -18 mwaka huu huenda
hukumu ya kesi hiyo kutolewa siku ya tarehe 18 mara baada ya mashahidi
kumaliza kutoa ushahidi wao ama kuendelea kikao kichacho iwapo mashahidi
wote zaidi ya 17 waliopo katika kesi hiyo watashindwa kufika mara ya
mwisho mtuhumiwa huyo kusomewa makosa yake mwaka jana.
Siku
ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la
kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO
huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani
hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku
waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika
kupigwa jambo lililoamsha hisia tofauti miongon
Katika kesi hiyo
hali ya kutofahamu imekuwa ikijitokeza na kufanya watu kuwa na maswali
zaidi baada ya 14 Februari Mwaka jana mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573
akiwa mahakamani hapo aliwatukana waandishi wa habari matusi ya nguoni
kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa muda si mrefu ataachiwa na
kupambana na waandishi mitaani.
Siku hiyo(Februari 14,2012) Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema
“mtapiga
picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatokahalafu
tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja kukutana
tu” alisema mtuhumiwa huyo.
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2
mwaka 2012 katika kijiji chaNyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa
akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment