MSANII wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kwamba anateseka na viashirio vya vita hasa baada ya CD zilizosambazwa na watu wasiojulikana wanaosema ni magaidi kudai kuwepo kwa vita nchini.
Msanii wa filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’.
Akipiga stori na gazeti hili, Jini Kabula alisema amekuwa akikesha
akimuomba Mungu ailinde nchi ya Tanzania na aiepushe na vita kwani tangu
amezaliwa mpaka alipofikia amekuzwa na amani na anajivunia kuwa
Mtanzania na anafurahi hivyo Watanzania wote wanatakiwa kudumu katika
maombi ili damu isimwagike kama hao magaidi wasiotakia mema nchi
wanavyoahidi.
“Namuomba Mungu usiku na mchana vita isitokee maana tumezoea amani
sasa ikitokea ukweli sijui tutafanyaje na tutakimbilia wapi hivyo ni
jukumu la kila Mtanzania kumuomba Mungu atuepushe na janga hilo,”
alisema Jini Kabula.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment