MAPENZI bwana! Mohamed Khalfan ambaye ni kikongwe wa miaka 78 mwenye ulemavu wa ukoma na mkewe, Habiba Shomari (68) hivi karibuni waliwashangaza watu baada ya kuamua kumwagiana mabusu hadharani.
Bw. Mohamed Khalfan(78) akimchumu mkewe, Bi. Habiba Shomari(68).
Tukio hilo lilijiri kwenye Kambi ya Walemavu wa Ukoma ya Chazi
iliyopo Kata ya Chazi wilayani Mvomero mkoani hapa ambapo kulikuwa na
kikao cha serikali za mtaa kutatua mgogoro wa ardhi.Akizungumza na Amani
huku akiwa na furaha, Mzee Khalfan alisema ndoa yake na mkewe ina miaka
60, walifunga mwaka 1955 mkoani hapa.
”Nampenda sana mpenzi wangu huyu. Nilifunga naye ndoa mwaka 55, ila
kwa bahati Mungu hakutujalia kupata mtoto hata mmoja.“Lakini pamoja na
kukosa mtoto hata wa dawa, tunaishi na mwezangu katika mapenzi mazito.
Kila siku namwona kama mchumba na yeye ananiona kama mvulana mbichi
kabisa,” alisema kikongwe huyo mwenye meno ya kuhesabu na kuwafanya watu
wawapongeze hasa ikizingatiwa kuwa, ndoa za siku hizi zikidumu miaka
miwili Mungu mkubwa!
Mzee Mohamed Khalfan akipozi na mkewe, Bi. Habiba Shomari.
Muda mwingi vikongwe hao walikuwa wakipelekeana midomo na kumwaga
mabusu mazito. Baadhi ya watu walisema kwa kizazi cha sasa kuna cha
kujifunza kwa vikongwe hao ingawa wenyewe walidai siri ya ndoa yao
kudumu ni kuvumiliana na kuheshimiana.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment