Nimelazimika kuanza na hiyo kauli hapo juu kutokana na unyeti wa habari yenyewe.
Nitakuwa namwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoikabili Tanzaniakwa kutumia mifano hai na kumbukumbu rasmi zilizopo Tanzania.
“Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani [“Godbless JonathanLema]. Haya maneno aliwahi kuyatoa Mbunge Lema, nayafananisha na kijitabualichokitoa Mh. January Makamba. Namheshimu sana [ Hata yeye anajua hilo!]lakini sina budi kusimamia ukweli na kukemea pale inapobidi!. Tanzania hii iliwahi kupata viongozi vijana wengi tu lakini historia inaonyesha waliwahi kuligarimu Taifa kutokana na ufinyu wa kufikiri na uharaka usiokuwa na tija!.Mfano Mh Raisi Kikwete, ndiye anaonekana kuwa Raisi kijana kuliko wote waliopata nafasi hiyo kwa siku za usoni lakini makubwa aliyoifanyia taifa hakuna ? aliwahi kuwa Waziri akiwa na miaka 38 tu?. Hivyo Umri sio kigezo cha kutushawishi kukupa uongozi. Uraisi sio sawa na kucheza filamu?.
Pili, Vijana tulio wengi hatuitaki ccm, yaani tunayavumilia sana majani hata hiyo rangi tungeiteketeza kabisa!!!!. Ukiona kijana yupo ccm jua lazima anapata mnofu? Vinginevyo hakuna au Baba yake aliwahi kuhudumiwa naccm hivyo na yeye anatega mpira?. Kutokana na sababu hii makini kabisa tunakuomba sana tena sana [Nakuheshimu sana Mkuu, hata wewe unajua hilo]usituharibie sifa ya ujana wetu kwa kutaka Makuu wakati bado unastahili kuwa nasubra baadae kama wataka nafasi hiyo ukaipata [ila kupitia chama kingine Mkuu].Kutunga kitabu kinachoelezea kuhusu Tanzania mpya ni maneno tu ambayo kwamtazamo wangu hayana uhalisia wowote ule.
Tatu,Nimewahi kuona watu wengi sana hasa walioko ndani yaccm wakikana maandiko yao yaliowahi kuwapa PHD, mfano DR. Harrison Mwakembe aliwahi kuzungumzia muungano wa serikali tatu kwenye kitabu chake lakini baadaye kupata tu ubunge hatimaye uwaziri kwenye uhalisia akaja kukana maandiko yake mwenyewe hivyo na hii Tanzania mpya ulioitazamia pindi utakapo pata nafasi basi itakuwa hivyo hivyo Mkuu , nakushauri egemea kwenye nini umewahi kuwafanyiaWatanzania na imebaki kama historia nasio utawafanyia nini tukikupa nafasi [uzoefu ni lulu Mkuu popote pale Duniani].Mh Nasari aliwahi kusema nanukuu ‘’CCMNI KAMA UKOO WA PANYA,BABA MWIZI MTOTO MWIZI’’ [Ukikasirika niombee].
Mwisho, Tanzania inahitaji kikongozi mwenye hofu ya Mungu [yaani mwenye hata kahistoria ka kuwa shehe,padre au hata mchungaji jamani] kutokana na sababu kuu moja kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani ambayo haina ‘’NationalPolicy’’ mtu akipata nafasi ya uwaziri tu anaweza kusema futa somo lahesabu kwa shule za msingi watasoma wakiwa sekondari kisa mwanae halipendi au kwasababu tu ya uswahiba na rafiki yako unaamua tu kuanzia kesho wewe utakuwa Mkuu wa wilaya [ kwa mfano tu wadau huyo jamaa alikuwa muuza chipsi leo anapata zali la kuwa mkuu wa wilaya]. Tunataka kiongozi mwenye hofu ya Mungu ili tutengeneze hizo policy kwanza maana nchi ipo pabaya.
Ila kiukweli nakupongeza kwa kutangaza nia na sio kwa kutoa kitabu, tuachie tukupime nini aulichowahi kuifanyi taifa hili Mkuu. Niombee kwa aliyekasirika. Nawatakia sikunjema
By
Elineema J Mosi
CPA[T]-Arusha,Tanzania.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment