Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:

fisadi



Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe.
Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.


Credit JamiiForims
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top