Msanii wa filamu anayeonekana kuwa moto, Ester Kiama.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Ester alisema wakati alipokuwa
nje ya fani alikuwa hapati usumbufu lakini sasa ameamua kuonyesha kipaji
chake anaonekana kama ameingia kujiuza kama wanavyofanya baadhi ya
wasanii wasiojitambua.“Mimi bwana siyo mburula, nimeingia kwenye filamu ili kuonesha kipaji changu na wala si kuja kuuza sura wala kujiuza, wanaojiuza ni haohao, hivi mimi naanzaanzaje?” alisema Ester ambaye amefanya kweli kwenye filamu ya Ngoma Ngumu inayotarajiwa kuingia mtaani wakati wowote.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment