Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.
Akizungumza na Ijumaa hivi karubini, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema
Diamond anaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi inayokuja lakini
akijaribu kutumia dawa hizo ataishia pabaya.“Tumeona wasanii wengi wa Tanzania ambao awali walikuwa wanafanya vizuri lakini baada ya kujaa sifa na kukutana na marafiki wengi pamoja na makundi wakazama kwenye dawa za kulevya na sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu wakati wenyewe wamejiharibia,” alisema Iron Lady.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wasani ambao awali walikuwa wakifanya vizuri kimuziki lakini baadaye
‘wakadrop’ baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya unga ni pamoja na Chid
Benzi, Ray C, Q Chiller, Lord Eyez, Msafiri Diof na wengine ambao sasa
wameshafariki.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment