
Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeanza rasmi kwa michezo miwili ya kundi A iliyochezwa kwenye siku ya ufunguzi (Jumamosi) ikizihusisha timu mwenyeji Equatorial Guinea na Congo Brazzaville pamoja na mchezo mwingine kati ya Gabon na Burkina Faso.
Katika mchezo wa kwanza Wenyeji Equatorial Guinea na Congo Brazzavile walitoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua ambapo timu hizi zilishambuliana kwa karibu dakika zote za mchezo.
Equatorial Guinea ndio walioanza kufunga kupitia kwa nahodha wao Emilio Nsue Lopez ambaye alifunga kwenye dakika ya 16 baada ya kupokea pasi toka kwa Ivan Zarandona.

Nahodha wa Eq.Guinea akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza kwenye mchezo wa ufunguzi wa Afcon.
Katika kipindi cha pili Congo Brazzavile waliendelea na mashambulizi mfululizo na walipata malipo ya juhudi zao baada ya bao safi lililofungwa na mshambuliaji Thievvy Bifouma .
Katika mchezo wa pili Gabon waliendeleza ubabe wao wa siku zote dhidi ya Burkina Faso kwa kuwafunga kwa matokeo ya 2-0 .

Aubameyang akishangilia baada ya kuiungia Gabon bao la kuongoza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Katika kipindi cha pili Gabon walifunga bao la pili kwenye dakika ya 72 mfungaji akiwa Malick Evouna akimalizia kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Frederic Bulot.
Matokeo haya yanamaanisha kuwa Gabon wanaongoza kundi A baada ya michezo ya kwanza wakiwa na pointi tatu huku Equatorial Guinea na Congo Brazzavil wakifuatia wakiwa na pointi moja kwa kila timu na Burkina Faso wanashika mkia wakiwa hawana pointi yoyote.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment