Taarifa Zinasema Prof Tibaijuka alifukuzwa kazi kutokana na ukosefu wa Maadili kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyodai,
Rais
Kikwete alitangaza kumfukuza kazi Mbunge huyo wa Muleba Kusini
(CCM)katika Mkutano wake wa Wazee wanaokaa mkoa wa Dar es Salaam
uliofanyika Mwanzoni mwa wiki liyomalizika jana Jijini Dar Es
Salaam,ambapo Rais Kikwete alisema Waziri huyo alipokea zaidi ya Bilioni
1.6 kutoka kwa Mbia wa Kampuni ya IPTL,Bwana James Rugimalira ambapo ni
Kinyume na Maadili ya utumishi wa Umma.
Licha ya
Profesa Tibaijuka kujinadi katika Mkutano wake na Wandishi wa Habari
aliouhitisha Alhamisi ya Wiki iliypita na Kujinadi kwamba hawezi
kujiuzulu kwenye Nafasi ya Uwaziri kwa Madai hakuhusika kwenye wizi wa
zaidi ya Bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa BOT.
Taarifa
za Kuaminika ambazo Mtandao huu umezipata zinasema Shinikizo la
kufukuzwa Prof.Tibaijuka limepewa nguvu na baadhi wa makada kutoka ndani
ya chama cha Mapinduzi akiwemo spika wa bunge Anna makinda ambao
wanamwona tishio katika harakati zake za kutaka kumrithi Rais
anayemaliza mda wake Jakaya kikwete mwakani 2015.
Kwa
Mujibu wa Chanzo chetu cha kuaminika kinasema Profesa Tibaijuka
alikutana na Rais Kikwete Ikulu Jijini hapa siku ya Jumatano iliyopita.
Ambapo katika mazungumzo yake Mtoa taarifa huyo anasema Prof Tibaijuka
alimueleza Rais Jakaya Kikwete Hatua kwa hatua jinsi Fedha zilivyotolewa
na Rugimalira hadi kupelekwa kwenye Akaunti ya shule ambayo ipo katika
Benki ya M,Sea View iliyoko Jijini Dar Es Salaam.
Aidha,katika Kikao hicho Rais Kikwete alikubaliana na Prof Tibaijuka na
akamtaka akaitishe mkutano na Waandishi wa Habari ili kutoa ufafanuzi wa
jambo hilo.
Na ndivyo Prof Tibaijuka akaitisha mkutano wake na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Hyatt Regency (KILIMANJARO)
Akilielezea hilo Ofisa mmoja wa Ikulu alinukuliwa na chanzo kimoja cha
Habari alisema baada ya kukutana na waandishi wa Habari, aliitwa tena
Ikulu,safari hii alikutana na Makamu wa Rais Dk,Mohamed Gharib Bilali na
Waziri Mkuu mizengo Pinda.
“Walipofika
hapa Ikulu,Prof Tibaijuka alikutana na Rais Kikwete Dk Bilali na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakamwambia kuwa Jinsi hali ya Hewa
ilivyochafuka ni vema akawapisha kwa kujiuzulu yeye alikataa”
“Akasema
hawezi kurudi tena kwa wananchi kuwambia anajiuzulu kufanya hivyo ni
kugeka jiwe ,kama wao wanamwona afai,basi wamfukuze kazi lakini siyo
kujiuzulu”aliileza Ofisa huyo Mwandamizi wa Ikulu ambaye akutaka Jina
lake litajwe mtandaoni.
Mbali na hivyo Taarifa Zengine ambazo Mtandao huu unazo pamoja na
Nyaraka mbalimbali zinamwonyesha Profesa Tibaijuka akipigania Uwaziri
Tangu Sakata hili lilivyokuwa Bungeni,lakini viongozi wa Bunge
wakiongozwa na Spika Anne Mkinda walimyima haki hiyo ndio maana Rais
Kikwete alipogundua kwamba Bunge lilimyima haki ya Kujitetea ndipo
akamtaka akajitete kwa wananchi.
Akiandika kwa Spika Makinda tarehe 20 Novemba 2014 Prof Tibaijuka
alisema “Pamoja na kuomba kuchangia kupitia Mhe Jestina Muhagama
–Katibu wa Bunge wabunge wa CCM-hadi sasa hakuna uhakika kama nitapewa
nafasi hiyo kabla hoja kufungwa’
Barua
hiyo kwenda kwa Spika Makinda ilikuwa na kichwa cha Habari hivi “Muda
wa Kujitetea mbele ya Bunge kufuatana a kutajwa kwa jina langu katika
Taarifa ya PAC –Issue ya Escrow
Katika
kile kinaoneka ni kwamba Spika Makinda alikuwa anataka kumsulubu Msomi
huyo alimjibu “ Suala hili ni kubwa sana,maelezo yako hapa Bungeni
hayataweza kukupa haki ambayo unastahili”
Alisema “Ushauri wangu jiandae Vizuri kusudi vyombo
vitakavyoshughulikia , vikikuita uweze kujitetea ufanye hivyo,sio humu
ndani”
Barua hiyo ya Anna Makinda ambayo ilimjibu Prof Tibaijuka aliandikwa Novemba 28 mwaka huu ina na Kumb Na.CBC.155/188/02/16 Hata
hivyo Profesa Tibaijuka hakukubaliana na majibu ya Makinda akandika
tena barua nyingine siku hiyohiyo,Profesa Tibaijuka akasema “Asante kwa
kujibu barua yangu.Ninakusihi sana unipe muda kuchangia kama unanitakia
kheri katika maisha yangu .Dunia inasubili Kauli Yangu”
Licha ya
kulalamika hivyo Spika Makinda akajibu Andishi hilo kwa kusema “Mh
Prof,Tibaijuka,Bunge hili haliwezi kukusaidia.Naomba ukubali kujiandaa
kwa hatua nyingine.maana wataibua hata mambo hayapo humu .Naomba
unisikilize”
Habari
zinasema Mbali na madai hayo Prof Tibaijuka amekuwa katika wakati mgumu
na Baada ya kukatalia Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC)kumlipa mshahara wa dola marekani 19,000 (elfu kumi na tisa kwa
mwezi) karibu zaidi ya Milioni 32.3 milioni mkurugenzi wa Shirika hilo
Nehemia Msechu.
Bodi ya NHC iliyoidhinishwa mshahara wa dola 19,000 kwa mwezi inaongozwa na mbunge wa kuteuliwa Zakia Meghji.
Kwa sasa Msechu anaweka kibindoni dola za 11oo0 zaidi ya milioni 18 pamoja namrupumrupu mengine kedekede.
BOFYA PLAY HAPA
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment