Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MSANII
wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake
zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana
huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana
ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa
ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo
ni mpenzi wake wa siku nyingi.
“Hizo picha ni sehemu ya vipande vya kwenye wimbo wa huyo mwanaume,
ukweli ni mpenzi wangu wa siku nyingi na anataka kunioa, ndiyo maana
kafikia hatua ya kujichora jina langu, sina kipingamizi, tunaomba Mungu
atufanikishe tufunge ndoa,” alisema.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment