Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

UCHAGUZI WA RAIS TUNISIA

Wananchi wa Tunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu kutokea vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011.
Mapinduzi hayo yalisababisha vuguvugu hilo la mabadiliko kutabakaa katika nchi nyingine za Kiarabu.

Miongoni mwa wagombea katika kinyang'anyoro hicho ni mwanasiasa mkongwe Beji Essabsi, aliyewahi kushika nafasi muhimu wakati wa utawala kabla ya kutokea mapinduzi.

Bwana Beji Caid Essabsi anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo ameahidi kurejeha kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.
Mpinzani wake wa karibu ni Rais wa mpito wa sasa Moncef Marzouki ambaye amejenga jina lake kama mpigania haki za binadamu na kama msimamizi wa moyo wa mapinduzi na anayetamani mabadiliko. Waziri wa Ulinzi wa Tunia Ghazi Jeribi amesema ana matumaini nchi itasonga mbele kidemocrasia.
(CREDIT: BBC SWAHILI)
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top