MIEZI michache kufuatia tamko la serikali kuzuia ngoma zinazokesha maarafu kama Kanga Moko kwa kukiuka maadili, imebainika kuwa ngoma hizo zinaendelea kufanya mambo kama kawa kana kwamba hazijakatazwa, Ijumaa limeshuhudia.
Baadhi ya wadada wakicheza ngoma ya kibao kata wakiwa ndani ya kanga moja.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
juzikati umebaini kuwa ngoma hizo ambazo wanawake hucheza wakiwa ndani
ya kanga moja, zinaendelea kufanyika kwa siri katika viunga mbalimbali
vya Jiji la Dar es Salaam.Chanzo makini kimevujisha habari kuwa,
wahusika wamekuwa wakipashana habari kupitia kwenye mitandao ya kijamii
kisha kukutana katika maeneo tulivu hasa kwenye fukwe na kufanya yao.
Wadada hao wakicheza ngoma hiyo huku wakipata sapoti kutoka kwa shabiki wa mchezo huo.
“Siku hizi wanatangaziana kwenye mitandao ya kijamii kisha mashabiki
na wadau wakubwa wa ngoma hizo wanakwenda kuwashuhudia,” kilisema
chanzo.Kuonesha kwamba kipo ‘serious’, chanzo hicho kilizidi kumwaga
ubuyu kwa kunyetisha siku ambayo ngoma hizo zilifanyika katika ufukwe
mmoja uliopo Mikocheni jijini Dar.
Wengine walishiriki mashindano ya umiss.
“Jumamosi hii (iliyopita) watafanya mambo
yao katika ufukwe wa...(anautaja jina) uliopo maeneo ya Mikocheni, kama
mtaweza fikeni muone jinsi usiku unavyotumika vibaya na ngoma hiyo,”
kilisema chanzo hicho.
Wadada hao wakizidi kutoa shoo.
Siku ya tukio, mapaparazi wetu walitinga
katika ufukwe huo na kujionea wadada watatu wakionesha ufundi wa kucheza
ngoma hiyo wakiwa wamevalia kanga moja kama kawaida yao.Mara baada ya
mapaparazi wetu kunasa picha kadhaa, walijaribu kuwauliza wadada hao kwa
nini wanakaidi agizo la serikali, lakini hawakuwa tayari kuzungumza
lolote.
Ma DJ wakinogesha 'beach party' hiyo.
Mapema mwaka huu, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), lilipiga
marufuku ngoma hizo kwa kuonekana hazina maadili na si utamaduni wa
Mtanzania.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment