Uaminifu ndani ya ndoa hujenga familia bora!!! Yes tumekutana
tena kwenye kona hii yaMapenzi na Uhusiano. Kama inavyojulikana wazazi wawili
ndiyo muongozo wa familia, baba akiwa kichwa cha familia akifuatiwa na mama. Siku
zote familia bora hutegemea muongozo mwema wa wazazi,
kwani wao ndiyo walimu wa
kwanza kwa mtoto. Siku zote watoto hujifunza kupitia wazazi wao wanachokifanya
ili nao wakitumie kama dira ya maisha yao pindi wakifikia umri wa kujenga
familia zao. Kama muongozo utakaowafanya waweze kuishi muda mrefu katika maisha
ya ndoa na kifo pekee ndicho kitakacho watenganisha. Katika maisha ya kila siku
ya mwanadamu hawawezi kuishi kama malaika, ipo siku wanaweza kukosana kwani
makosa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Ndiyo maana tumefundishwa kusamehe au
kuomba msamaha pale unapojua umekosa. Lakini kuna baadhi ya familia zimekuwa zikiwashirikisha
watoto wao katika matatizo yao pindi wakosanapo, ikiwamo kufokeana mbele yao pindi
wazazi wanapo tibuana. Mnashindwa kutafuta sehemu ya faragha na kuonyana kiutu
uzima, kama wazazi ambao siku zote watoto hutakiwa kujifunza mazuri kutoka kwenu.
Kufokeana mbele ya watoto mnawafundisha nini? Inapotokea baba au mama anapokuwa
akimtumia mtoto wake kujua kama mwenzake kuna kitu kibaya amefanya kwa kumuuliza:
“Ulipotembea na baba yako hakuzungumza na wanawake?” Au baba kukuuliza “Nilipokwenda
kazini mama yako alitoka au alizungumza na mwanamume?” Nina imani kwa mawazo
yenu unajiona mpo sawa kumbe sivyo, kwa mtindo huu inaonyesha ndani ya uhusiano
wenu hakuna uaminifu. Hamuwezi kumfanya mtoto kama mlinzi wa mmoja wenu. Hivi mnamfundisha
nini au ndiyo mnajionyesha jinsi gani msivyo aminiana. Kwani mtoto huamini
matatizo ndani ya familia ni msiba mzito ambao mwisho wake ni wazazi kutengana
na kuweka mpasuko katika maisha yake. Mzazi mwenye busara siku zote hukanyana
sehemu ya faragha ambayo humfanya mtoto aamini siku zote wazazi wake hawana
matatizo. Pia kama una wasiwasi na mwenendo wa mwenzako kwa nini usimwite mkae
chini na kutatua kwa busara, kwani hakuna mwanadamu aliyekamilika asilimia mia.
Familia bora ni ile ambaye inahakikisha matatizo yao hayaathiri watoto wao,
hutatua kwa busara huku wakizingatia watoto wao wanawategemea wao. Wazazi kuweni
walimu wema katika familia zenu ili kujenga familia yenye maadili mema.Loading...
Post a Comment