Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SWITCH ON

 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo,Vanessa Mdee,Nay wa Mitego na Barnaba wakishirikiana kuimba wimbo maarufu uliotumika kwenye tangazo jipya katika kufanikisha zoezi la uzinduzi huo.

 
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mbando (kushoto), akimkabidhi mmoja wa wadau aliyebahatika kujishindia simu.
 
Mtangazaji wa kipindi ya XXL cha Clouds FM,B12 (kulia),akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung S5 Missie Popular aliyoshinda kwenye bahati nasibu ya papo kwa papo kwenye zoezi la uzinduzi huo.
 
Nay wa Mitego akiwa kwenye pozi na mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria.
 
Prodyuza wa Fish Crabs Records, Lamar akiwa kwenye pozi na marafiki zake kwenye uziduzi huo.
 
B12, akiwa kwenye pozi na baadhi ya warembo waliokuwa wakielekeza wageni kwenye uzinduzi huo.
 
Msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee (wa kwanza kushoto) akiwa katika pozi na baadhi ya marafiki zake.
 
Joyce Kiria (kulia),akiwa katika pozi na mtangazaji wa kipindi cha Kambi Popote, Anton Kalugenzi.
 
DJ,PQ akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
 
Mchekeshaji maarufu Bongo, Evans Bukuku (kulia), akiwa kwenye pozi na mtangazaji wa Times FM, Moko Biashara.
 
Msanii wa Bongo Fleva Dayna Nyange akifuatilia kwa makini shughuli za uzinduzi huo.
 
Meneja Mkuu wa Global Publishers LTD,Abdallah Mrisho (wa pili kutoka kushoto),akiwa kwenye pozi na mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe (kushoto) mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchumvu (kulia) na Graphics Designer wa ITV.
 
Baadhi ya wasanii kutoka THT wakitumbuiza.
 
Baadhi ya memba wa mtandao wa G5click wakiwa kwenye pozi kwenye uzinduzi huo.
 
Vanessa Mdee akiwa katika pozi na mtangazaji wa Clouds TV, Shadee.
 Airtel yazindua huduma ya kipekee ya vifurushi vya data maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.
·        Airtel kuwapa suluhisho bora wateja katika huduma ya Internet
·        Wateja wa Airtel kufurahia inteneti bora kwa gharama nafuu
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua huduma kabambe ya Intaneti itakayojulikana kama SWITCH ON. Huduma hiyo ni maalum kwa watumiaji wa huduma za Interneti Tanzania ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kufuruhai huduma ya kipekee ya vifurushi vya data/intaneti maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”

“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’ watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako. Hii ni huduma inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI au MWEZI”

“Airtel Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea kufanikisha  hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku. Hivyo leo hii SWITCH ON nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza Nyakundi

 Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga, unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha intaneti maalum kwa kila simu”

‘Vilevile kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema Prisca.
  (GPL)

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top